Tuesday, May 7, 2019

Mfahamu kiongozi wa upinzani Afrika Kusini anayeandamwa na kivuli cha Mandela

Mmusi Maimane ndiye kiongozi wa kambi ya upinzani nchini Afrika Kusini.
Yeye ndiye kinara katika wa upinzani katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ambao wachambuzi wanauita ni harakati ngumu za kutaka kumng'oa rais Cyrill Ramaphosa madarakani.


    Japo utawala wa kibaguzi ulikomeshwa rasmi Afrika ya Kusini mwaka 1994, mfumo wa vyama vya siasa kwa kiasi kikubwa, mifumo ya vyama vya siasa nchini humo imejengeka kulingana na Ni dhahiri kuwa, kuchaguliwa kwa Maimane kukiongoza DA imekuwa ni moja ya mbinu za chama hicho kuonekana ni cha wote na si kundi fulani ama rangi fulani.
    "Uweledi wa kiuongozi si jambo la uzoefu tu," ameiambia BBC na kuongeza, "Je, nimekuwa kisiasa toka nilipopata cheo hicho? Jawabu ni ndio."
    Na hivi karibuni aliwaambia wapinzani wake ndani na nje ya chama hicho 'wafunge midomo yao' kwa kumkosoa kuwa yeye ni kibaraka ama hana uzoefu wa kutosha.
    Presentational grey line
    Democratic Alliance leader Mmusi Maimane.Haki miliki ya pichaAFP
    Mambo saba kuhusu Mmusi Maimane
    • Alizaliwa mwaka 1980 kitongoji cha Soweto, Johannesburg ambapo Nelson Mandela aliishi kwa miaka mingi.
    • Amesoma vyuo vikuu nchini Afrika Kusini na Wales, ana Shahada ya Uzamivu katika masomo ya Teolojia na Saikolojia.
    • Ameoa mwanamke wa kizungu Natalie, ambaye walikutana kanisani, na kukiri kuwa ilimchukua muda kukubaliana na jamii inavyochukulia tofauti yao.
    • Anaongea lugha sita.
    • Amekuwa akihubiri kanisani jijini Johannesburg mwishoni mwa wiki kwa miaka kadhaa sasa.
    • Alikuwa mshauri wa kibiashara kabla ya kuingia kwenye siasa, na kuwa msemaji wa DA mwaka 2011.
    • Alichaguliwa kuwa kiongozi wa kwanza mweusi wa DA mwaka 2015 akiwa na miaka 34.
    Presentational grey line
    'Mapambano ya kihistoria'
    "Usipoteze kura yako tena kwa mtu mweupe," katibu mkuu wa ANC hivi karibuni amewaambia wapiga kura kwenye kampeni, akikilenga chama cha DA.
    Maafisa wa ANC, na wale wa chama kidogo lakini chenye msimamo mkali cha Economic Freedom Fighters (EFF), kinachoongozwa na Julius Malema, wanakishambulia wazi wazi chama cha DA kuwa si upinzani bali watumishi wa "mabepari weupe," na Bw Maimane kuwa ni "mfanyakazi wa bustani" anayelinda maslahi ya wazungu wachache.
    Mwaka 2005, Maimane alifunga ndoa na mwanamke wa Kizungu ambaye alikutana naye kanisani miaka kadhaa nyuma. Wana watoto wawili, wakike na wakiume.
    Kwa sasa Maimane anasema harakati dhidi ya ubaguzi nchini humo ni "mapambano yake ya kihistoria."
    "Bizo ndizo harakati zinazotawala Maisha yangu na nitazipambania mpaka siku nakufa," ameiambia BBC.
    Democratic Alliance members await the arrival of Mmusi Maimane on the campaign trail in Durban on 17 March 2019.Haki miliki ya pichaAFP
    Image captionCham cha DA kinataka kujivua dhana kuwa ni cha watu weupe waliowachache nchini Afrika Kusini
    Lakini mapambano hayo ya Maimane si kwa vyama pinzani tu, bali hata ndani ya DA.
    "Chama cha DA kililazimika kubadilika. Inabidi tuendelee kukibadilisha chama," amesema Maimane.
    Je anafanikiwa katika hilo?
    Wakosoaji wake wanasema uthabiti wa chama hicho umejengeka katika misingi yake ya kupambana kisera na utawala bora. Na kwakuwa Maimane aliingia uongozini akiwa hana uzoefu wowote, hivyo hana mchango mkubwa katika kukiimbarisha chama.
    Lakini kwa Maimane na wafuasi wake, wanasisitiza kuwa chini ya uongozi wake, chama hicho kimetanuka na kupenya katika maeneo na "jamii ambazo isingeweza kuzifikia hapo kabla."
    Kujikita katika siasa za uchumi
    Siku chache zijazo zitaamua mustakabali wa Maimane kisiasa.
    Mapambano makali zaidi yapo kwenye jimbo Tajiri zaidi nchini humo la Gauteng.
    Mmusi Maimane pictured with his wife, Natalie, in Cape Town ahead of the State of the Nation address on 16 February 2018.Haki miliki ya pichaAFP
    Image captionMmusi Maimane na mke wake, Natalie
    Chama cha DA ambacho tayari kinalishikilia jimbo la Western Cape, endapo kitaweza kuwashusha ANC mapaka chini ya 50% jimboni Gauteng, basi wataweza kuingia kwenye serikali ya mpito ya jimbo hilo.
    Ingawa kwa mwaka huu kura zote za maoni zinaonesha kuwa ANC watashinda uchaguzi, mchuoano wa Gauteng unatazamiwa kuamua uchaguzi wa kitaifa wa mwaka 2024.
    Katika miaka ya mwisho ya utawala wa rais aliyejiuzulu Jacob Zuma, chama cha ANC kilipoteza Imani miongoni mwa raia wengi wa nchi hiyo kutokana na kushamiri kwa kashfa za rushwa na ufisadi.
    Japo kwa sasa chama hicho kimeanza kurejesha Imani polepole chini ya rais Ramaphosa.

    Hata hivyo, Muimane anaamini ANC haiwezi kubadilika na imevunjika vipande vipande ambavyo haviwezi kuungika tena na kuwa kitu kimoja.
    Lakini pia nafahamu fika kuwa ni mapambano makli zaidi kuwaaminisha waliowengi nchini Afrika Kusini kuwa yeye na chama chake cha DA ndiyo mbadala na jibu kwa matatizo ya nchi.
    "Ninawaasa na kuwaomba Waafrika Kusini kuwezesha siasa za mrengo wa kati (chama cha DA) kushinda. Mabadiliko huwa hayapendezi sana mwanzoni, lakini tunayahitaji," amesema Maimane.
     za raia wake.

    No comments:

    Post a Comment