Inaelezwa kuwa mwimbaji wa miondoko ya RnB Chris Brown ameamua kuja na ngoma 30 ambazo zitakuwepo ndani ya album yake ijayo “Indigo” ambayo imetajwa kuachiwa June mwaka huu baada ya kutimiza miaka 30 Mei 5,2019.
Chris Brown ametupa taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo imeeleza kuwa mkali huyo wa R&B ameweka rekodi ya kufikisha wiki 400 ndani ya chart za album (Billboard 200) baada ya album yake iliyopita ‘Heartbreak On A Fool Moon’ kufikisha wiki ya 77 mpaka sasa tangu itoke October 31, 2017 ikiwa na jumla ya ngoma 45.
No comments:
Post a Comment