Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Wednesday, May 8, 2019

MESSI AZIOTA 4-0 ZA LIVERPOOL


Bao la mapema la Divock Origi ndilo lililoamsha mashetani wa The Reds


Liverpool ilionyesha mchezo mzuri katika historia yake baada ya kutoka nyuma na kuilaza Barcelona kwa jumla ya magoli 4-3
Baada ya kupoteza kwa magoli 3-0 katika uwanja wa Nou camp , Liverpool ililipiza kisasi wakati Divock Origi alipoiweka kifua mbele timu hiyo.
Georginio Wijnaldum alifunga magoli mawili katika dakika mbili ili kusawazisha

Origi baadaye alifunga goli lake la pili na la nne kwa upande wa Liverpool kutokana na kona iliopigwa kwa haraka ili kukamilisha ushindi mkubwa.
Liverpooll sasa huenda ikacheza dhidi ya Ajax ama Tottenham katika fainali ya kombe la vilabu bingwa mjini Madrid mnamo tarehe mosi mwezi Juni.
Ilikuwa mazingaombwe kwa Barcelona ambao walicharazwa 3-0 na Roma katika mkondo wa pili wa robo fainali ya kombe hilo mwaka uliopita kutokana na goli la ugenini , baada ya kushinda mkondo wa kwanza 4-1.

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp alijawa na furaha chungu nzimaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp alishindwa kujizuia baada ya kushuhudia kikosi chake kikitoka nyuma na kuwalaza mabingwa hao wa La Liga .
''Mechi yote kwa jumla ilikuwa zaidi' , alisema Klopp.
''Kushinda ni vigumu lakini bila jibu , sijui waliwezaje kufanikiwa''.

Ni mazingambwe kwa Messi ambaye hakuaminiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Lakini kwa Liverpool ilikuwa kumbukumbu nyengine ya matokeo mazuri ya Ulaya ambayo yanafananishwa na ushindi wao dhidi ya AC Milan katika fainali ya 2005 na ushindi wao wa 4-3 dhidi ya Borussia Dortmund katika uwanja wa Anfield miaka mitatu iliopita.
Ni mara ya kwanza tangu 1986-wakati Barcelona ilipoilaza Gothenburg katika kombe la Ulaya-ambapo timu ilitoka nyuma kwa magoli matatu kushinda nusu fainali ya michuano hiyo.
Baada ya magoli hayo manne mashabiki wa nyumbani walisimama wakiishabikia timu yao katika dakika za mwisho huku wachezaji wa Barca walioshangazwa wakishindwa kujibu mashambulizi ya Liverpool.
Kipenga cha mwisho kilipopulizwa kilileta sherehe kubwa ndani ya uwanja na katija maeneo ya mashabiki.
Liverpool imefanikiwa kutoka nyuma na kushinda katika siku za nyuma , hususana wakati waliposhinda taji lao la tano mjini Istanbul lakini ushindi huu dhidi ya barcelona ndio mkuybwa katika historia ya klkabu hiyo wanapojiandaa kucheza dhidi katika fainali mji Madrid.
Sio mara ya kwanza kwa Barcelona kuadhibiwa kwa kiwango hiki, baada ya kufungwa 3-0 na Roma katika robo fainali mwaka uliopita baada ya kushinda mkondo wa kwanza 4-1 hivyobasi wataendelea kusubiri kutinga fainali tangu 2015.
Walichezewa katika kila safu na ijapokuwa walipata fursa kadhaa hawawezi kudai kwamba walihitaji kushinda.
Kulikuwa na kipindi kifupi katika kipindi cha kwanza , wakati mabingwa hao wa La Liga walipoamka na kuanza mchezo wao mzuri na katika kipindi cha dakika tano kipa Allison alimnyima Messi na Phillipe Coutinho huku Jordi Alba akilazimika kutoa pasi wakati ambapo alikuwa amesalia na kipa huyo kucheka na wavu.
Messi ambaye alikuwa mchezaji mwenye kasi kubwa wiki moja iliopita alishindwa kutawala hususan katika kipindi cha pili wakati magoli ya Wijnaldum yalioposawazisha.
Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez pia alipotea huku mchango wake ukionekana wakati ambapo alizomwa mara kwa mara na mashabiki ambao walizoea kumuabudu.
Alikuwa na fursa nzuri katika kipindi cha pili , wakati Messi alipompatia pasi nzuri huku Liverpool ikiwa 1-0 usiku huo lakini Allison alikuwa macho na hiyo ndio iliokuwa nafasi ya mwisho wageni hao kutekeleza tishio lolote.

Georginio Wijnaldum alifunga goli la PiliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Georginio Wijnaldum alifungoli la tatuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mchezaji bora-Sadio Mane Liverpool


Ilikuwa vigumu kumtambua jmchezaji bora lakini Sadio mane alihitaji kupewaa taji hiloHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Takwimu za Liverpool kombe la klabu bingwa

  • Liverpool imefanikiwa kutinga fainali ya tisa katika klabu bingwa Ulaya huku Real Madrid wakifika mara 11 nayo Bayern wakitinga mara 10.
  • Ndio timu ya kwanza katika ligi ya Uingereza kutinga fainali mara mbili mfululizo tangu Manchester United mwaka 2008 na 2009.
  • Hii ni mara ya nne kwa timu kutoka nyuma ikiwa 0-3 katika mkondo wa kwanza wa klabu bingwa ili kusonga mbele. Barcelona pia iliondolewa kama hivyo mwaka uliopita dhidi ya Roma.
  • Barcelona kufikia sasa wameondolewa katika michuano mitatu kati ya minne ya nusu fainali ya klabu bingwa iliopita.
  • Mabingwa hao wa La Liga walishindwa kwa magoli mengi dhidi ya klabu ya Uingereza katika mashindano yote ya Ulaya.
  • Beki wa kulia Trent-Alexander Arnold ametoa usaidizi mara 14 katika mashindano yote msimu huu , zaidi ya wachezaji wengine wa Liverpool.
  • Divock Origi alifunga magoli yake ya kwanza ya klabu bingwa na hivyobasi kuwa mchezaji tofauti wa 50 wa Liverpool kuifungia Liverpool.
  • Georginio Wijnaldum ni mchezaji wa kwanza wa Liverpool kufunga magoli mawili kama mchezaji wa ziada tangu Ryan Babel dhidi ya Besikitas 2007.
  • Pia ni mchezaji wa kwanza wa ziada kufunga katika mechi moja dhidi ya Barcelona katika michuano hiyo.
  • Lionel Messi alijaribu kufunga magoli matano mbali na kutengeneza pasi tatu katika mshambulizi yote ya Barcelona dhidi ya Liverpool katika mechi hiyo

Tuesday, May 7, 2019

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 07.05 2019: Fernandes, De Ligt, Pogba, Dybala, Lo Celso, Bale, Trippier, Martial

Kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba, 26, anafikiria kuhamia Real Madrid mwisho wa msimu , lakini matumaini yake ya kuhamia klabu hiyo yatategemea Man United kupunguza thamani yake ya £160m. (Telegraph)
Pogba atalazimisha kuondoka hata iwapo Man United itakataa kumuuza. (ESPN)
Manchester City inakaribia kuingia makubaliano na kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, huku klabu hizo zikijadiliana kuhusu dau la kati ya £50m na £60m kwa mchezaji huyo wa PortuPaul Pogbamwenye umri wa miaka 24. (Sky Sports


Beki wa Ajax Matthijs de Ligt, 19, amekataa uhamisho wa kuelekea Manchester United wenye thamani ya £60m. (Star)
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amejiunga katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Brazil na Ajax David Neres kwa dau la £35m . (Sun)
Manchester United iko tayari kuanza uhamisho wa wachezaji inaowalenga ili kuimarisha kikosi hicho na tayari imewasiliana na Juventus kuhusu kumsaini mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala kwa dau la £85m(Calciomercato, via Mail)
David Neres
Tottenham na Everton wanamuwania mshambuliaji wa Real Betis Giovani Lo Celso, 23. (Sun)
Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29, ameambiwa kwamba hatakikani katika klabu ya Real Madrid katika mkutano wa ana kwa ana na mkufunzi Zinedine Zidane, lakini bado anataka kusalia katika klabu hiyo . (Mail)
Mkufunzi wa Napoli na aliyekuwa mkufunzi wa zamani wa Chelsea Carlo Ancelotti ametoa ishara za kutaka kumsajili winga wa Mexico Hirving Lozano, 23, ambaye amehusishwa na uhamisho wa Manchester United. (Calciomercato)
Kieran Trippier
Ancelotti amekataa kupiga madai ya kutaka kumsajili beki wa Tottenham Kieran Trippier, 28, baada ya mke wa mchezaji huyo wa Uingereza kuonekana akitafutia shule watoto wake mjini Napoli.. (Talksport)
Winga wa Ufaransa Anthony Martial, 23, anakabiliwa na changamoto ya kumshawishi mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer kwamba ana kandarasi ya muda mrefu katika klabu hiyo.. (Mail)
Solskjaer atasikiliza kuhusu ofa za Martial zitakazowasilishwa kutokana na tabia yake mbaya wakati wa mazoezi.. (Sun)
Maajenti wa Martial wameandika katika mtandao wa instagram ili kutetea rekodi ya mshambuliaji huyo wa Man United huku kukiwa na ukosoaji kuhusu kiwango cha mchezo wa uwanjani Old Trafford.(Manchester Evening News)
Arsene Wenger
Mkufunzi wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger, 69, amekataa ofa nyegine ya pili kuifunza klabu ya Fulham, baada ya kukataa kwa mara ya kwanza mnamo mwezi Novemba kabla ya kumuajiri Claudio Ranieri.. (Mail)
Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Antonio Conte anasema kuwa kuna asilimia 60 kwamba huenda akarudi kufunza katika ligi ya Serie A msimu ujao.. (Le Iene - in Italian)
Newcastle United imekuwa ikimchunguza kiungo wa kati wa Uingereza na Coventry Tom Bayliss, 20, kabla ya kumsajili mwisho wa msimu huu . (Chronicle)
Kipa wa Poland Marcin Bulka, 19, anatarajiwa kuondoka Chelsea mwisho wa msimu huu na atatia saini kandarasi ya mapema na Paris Saint-Germain. (Goal.com)
Beki wa zamani wa Uingereza Gary Cahill, 33, ambaye anaondoka Chelsea mwisho wa msimu huu , anasema hajaridhika na soka ya kiwango cha juu na anasisitiza anaweza kuendelea kucheza. (Talksport)

TETESI ZA SOKA JUMATATU

tetesi
Tottenham inajiandaa kucheza msimu ujao bila ya kiungo wa kimataifa wa Denmark kiungo Christian Eriksen, 27, na wanaelekea kumsajili kiungo wa Ajax Donny Van de Beek 22, ambaye pia anatakiwa na Real Madrid na Bayern Munich.(Mirror )
Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri ameitaka klabu yake kumsajili moja kwa moja mshambuliaji Gonzalo Higuain ambaye anaichezea Chelsea kwa mkopo akitokea Juventus ili kuimarisha kikosi chake. (Goal.com)
Mchezaji wa kimataifa wa England Danny Welbeck, 28Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMchezaji wa kimataifa wa England Danny Welbeck, 28
Mchezaji wa kimataifa wa England Danny Welbeck, 28 hatopewa mkataba mpya na klabu yake ya Arsenal na ataondoka akiwa mchezaji huru katika dirisha lijalo. (Sky Sports)
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane atamruhusu kiungo Luka Madric kuondoka. (AS)
Mchezaji wa kimataifa wa Venezuela Salomon Rondon, 29 ambaye anachezea Newcastle kwa mkopo amewaambia Magpies kutoangalia umri wake na kumnunua kwa sababu anafanana na mvinyo.(Mirror)
Winga wa Nice, Allan Saint-Maximin, 22, anayewaniwa na Arsenal na amefungua njia ya kujiunga na AC milan baada ya nafasi ya kujiunga na klabu hiyo mwezi januari kushindikana.
Tony Mowbray
Image captionTony Mowbray
Meneja wa Blackburn Tony Mowbray amejiweka mbali na ripoti zinazozungumzwa kuhusu klabu yake kutaka kumsajili goli kipa wa zamani wa England Joe Hart, 32.
Mlinzi wa Chelsea Kurt Zouma ambaye anacheza kwa mkopo katika timu y a Everton anatarajiwa kurejea Stamford Bridge kuanza maandalizi ya msimu mpya ingawa The toffees wanataka kumsajili kwa mkataba wa kudumu .
Nahodha wa Chelsea Gary Cahill, 33Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionGary Cahill, 33
Nahodha wa Chelsea Gary Cahill, 33 na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England amemshambulia meneja wake Maurizio Sarri kwa kusema ameshindwa kumuonyesha heshima mchezaji huyo mkongwe wa Chelsea.
Klabu wa Celtic imetoa ofa kwa meneja wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho, 56 kwa kumpa nafasi ya kuwa meneja wa klabu hiyo msimu ujao. (Sky Sports Italia, via Express)