Met Gala 2019: Watu maarufu waonyesha mitindo yao ya kipekee kwenye zulia jekundu
Tamasha la Met Gala, tukio lenye faida kwa Taasisi ya mavazi -Costume Institute at the Metropolitan Museum ya Art in New York, hutajwa kama moja ya tukio kubwa kabisha duniani la fasheni.
Linafahamika kwa orodha yake ya majina ya wageni maarufu wanaoalikwa , kushiriki ni gharama kubwa na zaidi ya yote nguo zinazovaliwa ni za ghali mno kulingana na mada ya mwaka.
Mwaka huu, mada hiyo ilikuwa ni Camp: Waraka kuhusu mitindo ya mavazi - inayoendana na onyesho lijalo katika katika Met, picha zilipigwa kwa kuzingatia inshailiyoandikwa na mpigapicha Susan Sontag mwaka 1964 iliyofahamika kama - Notes on Camp.
Na kumuonyesha kila mshiriki jinsi mambo yanavyopaswa kufanyika mwanzo kabisa alikuwa ni muimbaji Lady Gaga, aliyewasili akiwa ametinga gauni la rangi ya waridi linalopeperuka haikuonekana hivyo alipoingia.
No comments:
Post a Comment